Thursday, 16 February 2017

MESSAGE ZA MAPENZI



     Message za      Mapenzi

Kupendwa au kependana ni jambo ambalo limekubalika katika jamii. Mapenzi kati ya wapendanao hujengwa kwa maneno matamu ya kuufurahisha mtima wa mchumba wako au yeyote youle unayemtumia arafa za mapenzi.
Kwa arafa nzuri za mapenzi zitakazomsisimua na kumburudisha mpenzi wako, soma makala haya hadi mwisho.
Message za mapenzi
  1. Naweza kukupa masikio yangu usikilizie, mabega yangu ulalie, miguu yangu utembelee na mikono yangu ushikie. Kitu kimoja  siwezi kukupa ni moyo wangu kwani tayari nilishakupa zamani.
  2. Nimezihifadhi hisia zako katika moyo wangu. Nakuahidi kuwa sitawahi punguza upendo wangu kwako. Kwa hivyo, tunza arafa hii ya ahadi kwenye simu yako, ili iwe kumbukumbu kila uisomapo! “nakupenda sana malaika wangu.”
  3. Wewe ni wapekee na ninakupenda sana. Sifikirii kukusaliti na wala sina wazo la kukutenda mambaya. Nakuomba tuendelee kupendana siku zote Mpenzi wangu.
  4. Nashtakiwa kwa kumpenda msichana fulani aliyeutesa sana moyo wangu. Mahakama imenihukumu kifo na kifaa kitakachoninyonga ni upendo. Lakini Raisi Mapenzi amenisamehe na akaamrisha nimehukumiwe kuwa mwaminifu kwa mschana huyo na kumpenda milele. Nakupenda mpenzi wangu.
  5. Natamani niwemachozi machoni mwako ambapo ningeteremka na kuishia midomoni mwako. Lakini sitamani kamwe uwe machozi machoni mwangu. Maana nitakupoteza kila muda niliapo.
  6. Aha! Cjui ni kwa nini nina hamu ya kulifaidi penzi lako kiasi hiki? Natamani uwe karibu nami unipime ugonjwa huu na pia unitibu. Kwani wewe ndiye daktari wa kipekee ninaye mwamini kwa moyo wangu wote. Nahisi nazidi kuchanganyikiwa kwa kukosa penzi lako.
  7. Thamani ya penzi lako ni kubwa kwangu, siwezi kuifananisha na chochote katika ulimengu. Kwa hivyo sina budi kumshukuru muumba, kwa kunipa mpenzi mwema anayezijali hisia zangu na kunipenda kwa dhati. Usiache kunipendampenzi wangu.
  8. Kila tunapokuwa chumbani nawe mpenzi wangu, huwa natamani niwe mbunifu na pia huwa najitahidi kuepuka udhaifu ili penzi langu kwako lisikukifu. Kwa hivyo, endelea kulifurahia peni langu mpenzi.
  9. Mapenzi yana raha na ni matamu pia. Hamu ya kuwa nawe hainiishi kwa sababu siku zote wanipa raha. Umuhimu wako kwangu haufananishwi na chochote duniani. Moyoni mwangu unang’aa kama nyota ya jaha. Nakusihi ulitunze penzi letu mpenzi wangu.
  10. Moyo wangu unadhamiria kukupenda wewe pekee. Kupenda kwa dhati siku zote bila pigamizi lolote lile. Kwa hivyo, nipende nami nitakupenda na tudumishe mapenzi ya dhati.
  11. Niruhusu nitamke neno ambalo halina gharama na hutumiwa vibaya na kwa wengi halina thamani wala maana. Siwezi kuliandika neno hili kwa karatasi wala kulitamka neno hili pasi na kukumbuka uso wako. Ningependa kukujulisha ya kwamba neno hili hutufanya mimi na wewe tuwe pamoja japo tuko kusi na kasi. “ Nupenda mpenzi wangu.”
  12. Uliwahi kufikiria upendo ni nini? Upendo ni jawabu kuwa kila mmoja anataka… kwa hivyo, upendo ni lugha. Mimi na wewe tunaongea, lakini hatuwezi kuununua upendo. Upendo ni kama uchawi safi na ndiyo siri kuu ya maisha mazuri. Nakupenda Mpenzi.
  13. Zidhamirii kuukabidhi mtima wangu kwa mwingine ila wewe. Nataka uelewe kuwa wewe ni wa kipekee maishani mwangu. Nipende mpenzi na nahaidi kuwa nitalienzi penzi lako daima.
  14. Mapenzi ni kama utoto, deka ulie na tikumbebeleza mpenzi wangu. Penzi ni kama zawadi, tabasamu na ulibusu shavu langu halafu uniambie kiasi gani wanipenda. Lakini, jua kuwa jina lako limeandikwa katika moyo wangu kwa wino usiofutika.
  15. Nimezuguka sana nikiyaangaza macho angalau nipate mschina mrembo wa kumpa moyo wangu, moyo uliojaa upendo, alile tunda lililomo huku nikimpa mahaba ya dhati. Kwa bahati nzuri, uliuteka moyo wangu na nishaukabidhi kwako. Tulitunze penzi mpenzi wangu.
  16. Je, unakubali au unakana kwa mujibu wa sheria za mahakama ya mapenzi kifungu cha mahaba unahukumiwa kunipenda siku zote? Utakubali kukata rufaa kwa sababu hujatendewa haki?
  17. Wengi husema mapenzi ni upepe, mimi sivumi na kupotea. Pia wakasema kuwa mapenzi ni mahaba, mimi sili nakamaliza. Wakamalizia na kusema kuwa mapenzi ni raha, na mimi siwezi kuipeza. Nipenda nami nikupende, tupendane tufunzane utamu wa mapenzi.
  18. Japo mbinguni sijafika, lakini najua vizuri mtoto umeumbika kama malaika. Nina uhakika kwamba kila mwanamume akikuona hana budi kutokwa na udenda. Naomba uniruhusu nikueleze ninavyohisi moyoni mwangu kwani nimeshindwa kuficha kukueleza jinsi ninavyokupenda. Amini ninakupenda sana.
  19. Najua kuwa utarejea nyumbani ukiwa umechoka. Tafadhali badilimavazi yako, halafu uingie bafuni kujimwagia maji. Nitamani nikusaidie kuusugua mgongo wako na pia nikuandalie chakula, lakini siku haijawadia mpenzi.
  20. Mapenzi yanalewesha ingawa si pombe, yanapoesha ingawa si dawa. Mpenzi humfanya mtu alie na ingawa si katuni, inkufanya uchecke. Ni mimi tu mwenye mapenzi ya dhati kwa, nipende nami nikupende, tupendane siku zote.
  21. Weupe wa mapenzi yako kwangu ni kama mwezi angani. Mahaba na ucheshi wako siwezi kufananisha na chochote. Ninaposema kupata mfano wako hautawahi kutokea, niamini. Elewa kuwa nakupenda na sikuachi asilani.
  22. Sijui nikueleze vipi ili uelewa kuwa moyo wangu umejaa penzi lako. Kila nifikiriapo mbona una walakini na huniamini ninaposema kuwa ni wewe pekee ninayekupa mahaba yangu. Tafadhali mpenzi, rudisha imani yako na uamini ni wewe ninayependa pekee duniani.
  23. Kwa kawaida, busu la amani hubusiwa kwa mashavu, busu la mafanikio usoni, busu la upendo ndomoni, na busu la mapenzi shingoni. Je, ungependa nikupe busu gani mpenzi?
  24. Mpenzi, elewa kuwa ni wewe sababu ya huu usingizi. Najilaza kitandani nikiamini kuwa tutakutana kwenye njozi, njozi ya kuyaenzi mapenzi yetu. Nakupenda sana.
  25. Najua umechoka sana hata akili yako. Huu ndio wakati wako wa kupumzika na ninakutakia usiku mwanana. Lakini wacha moyo wako uwe macho ya kumuona anayekupenda kwa dhati. Pokea busu mpenzi wangu.
  26. Natamani sana kuyaona macho yako yakifumbua, pia nataka kuzisikia sauti zako za ndoto zako. Natamani zaidi kukuona ukijigeuza kitandani. Nikukumbuka busu lako la kunitakia usiku mwema, nakutamani wewe.
  27. Mpenzi, najua wanaokutamani ni wengi lakini elewa kwamba ni mimi tu kati yao mwenye mapenzi ya dhati. Ziba masikio usiwasikie kamwe, nia yao ni kutugombanisha. Nipende daima mpenzi wangu.
  28. Utamu wa samaki ni kula na wali, na usikimbie nyuki ukakosa asali. Ni mimi tu niliyeshughulika kukujulia hali. Umeshinda aje sakafu ya moyo wangu?
  29. Furaha yangu ni kuwa nawe kwani u zaidi ya mboni yangu. Najisifu kuwa nawe maishani mwangu na ninaamini siku itatokea ilikuwa karibu nawe mpenzi wangu, unisahaulishe machungu na karaha za huu ulimwengu.
Tumia arafa hizi za mapenzi zitakuwezesha kuufurahisha moyo wa umependaye.
Publicado 

Deja un comentario

Tu dirección de correo electrónico no será publicada. Los campos obligatorios están marcados con *




1 comment:

  1. kama ungependa kuokoa uhusiano/ndoa yako basi nitakupendekeza kwa Dk Dawn. alinisaidia kurejesha nyumba yangu baada ya miezi 11 ya utengano mkali kati yangu na mume wangu. Nilielekezwa kwake na dada yangu mkubwa wakati ndoa imeisha, akarudisha amani na furaha katika ndoa yangu, pia amesaidia marafiki zangu wengine na wanaishi kwa furaha kwa msaada wa Dk Dawn,
    Wasiliana naye ikiwa unahitaji usaidizi wa kurejesha uhusiano/ndoa yako/ ikiwa unataka kupata mimba au kuponya aina yoyote ya ugonjwa:
    Dk Dawn hatawahi kukukatisha tamaa:
    Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com
    WhatsApp: +2349046229159

    ReplyDelete